Hebrews 6:13-17

13 aMungu alipompa Ibrahimu ahadi yake, kwa kuwa hakuwepo mwingine aliyekuwa mkuu kuliko yeye ambaye angeweza kuapa kwa jina lake, aliapa kwa nafsi yake, 14 bakisema, “Hakika nitakubariki na kukupa wazao wengi.” 15 cIbrahimu naye, baada ya kungoja kwa saburi, alipokea kile kilichoahidiwa.

16 dWanadamu huapa kwa yeye aliye mkuu kuwaliko, nacho kiapo hicho huthibitisha kile kilichosemwa na hivyo humaliza mabishano yote. 17 eMungu alipotaka kuonyesha kwa udhahiri zaidi ile asili ya kutokubadilika kwa ahadi yake kwa warithi wa ahadi, aliithitibisha kwa kiapo.
Copyright information for SwhKC